Huduma zetu
Mikopo
Mafunzo
Tafiti
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea ni Taasisi ya Serikali inayotoa mafunzo ya elimu ya; fedha, ujasiriamali na kujitegemea pamoja na mikopo kwa Vijana na Wanawake ili kuwawezesha kujiajiri na kujitegemea kiuchumi.
Wazo la kuanzisha Mfuko huu lilitolewa na hayati Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Moringe Sokoine kwa lengo la kuwasaidia wananchi kujitegemea kupitia shughuli za uzalishaji mali hasa katika maeneo ya kilimo,uvuvi,ufugaji na viwanda vidogo vidogo.Wazo hili lilikuwa linakusudia kutekeleza sera ya “Nguvu kazi”.
Kujenga uwezo kwa Vijana na Wanawake kwa kuwapatia huduma bunifu za kifedha na zisizo za kifedha kupitia wafanyakazi weledi, ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa walengwa.
Taasisi ya serikali inayoongoza katika kutoa huduma za kifedha kwa Vijana na Wanawake katika kuleta mabadiliko bora ya kiuchumi Tanzania.
- Kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana waliohitimu vyuo vya ufundi stadi na wanawake wajasiriamali walio katika sekta ya uzalishaji kwa lengo la kukuza mitaji yao ili kuongeza kipato na ajira miongoni mwao.
- Kusaidia jitihada za serikali za kuendeleza jamii ya watanzania kiuchumi ili kuleta maisha bora na maendeleo yaliyokusudiwa katika jamii
- Kutoa elimu ya ujasiriamali shirikishi kwa kundi la walengwa ili waweze kukabiliana na nguvu za soko pamoja na ushindani wa kibiashara Kuwajengea walengwa uwezo kwa kuendeleza na kuboresha fani walizosomea kwa ustawi wa jamii ya watanzania.
- Wananchi wenye miradi ya uzalishaji mali.
- Wananchi wenye ari na nia ya kujitegemea kiuchumi.
- Vijana na Wanawake wazalishaji mali wanaohitaji mikopo ya kuboresha ama kuanzisha miradi ya kiuchumi.
- Wahitimu wa vyuo vya ufundi stadi wenye taaluma na nia ya kuanzisha miradi ya kujiajiri.


