Mkopo wa Umoja

Huu ni mkopo wa kifedha unaotolewa kwa vijana waliohitimu katika Vyuo vya VETA na wale waliopata mafuzo kutoka SIDO na vyuo vingine vya ufundi stadi.

Vigezo vya Kupata Mkopo
  1. Uwe na umri kati ya miaka 18-45
  2. Uwe umehitumu katika vyuo vya ufundi stadi na kupatiwa cheti
  3. Uwe tayari kujiunga katika kikundi cha watu watano na kudhaminiana
  4. Uwe na shughuli za uzalishaji ama uwe tayari kuanzisha shughuli kulingana na masomo ya ufundi stadi uliyosomea
  5. Uwe na kitambulisho cha Taifa ama kadi ya mpiga kura
  6. Uwe na mahali maalumu pa kufanyia shughuli yako
  7. Uwe katika eneo la maradi wa PTF
  8. Uwe na historia nzuri ya ukopaji
Viwango vya Mkopo
  • Mkopo wa chini TZS 100,000
  • Mkopo wa juu TZS 5,000,000
  • Muda wa urejeshaji ni kati ya miezi 6-12

Mkopo wa Jiendeleze

Unamlenga mjasiriamali aliyehitimu mkopo wa Umoja. Mjasiriamali mwenye mradi wa uzalishaji na aliyehitimu mzunguko wa mkopo wa Umoja.

Vigezo vya Kupata Mkopo
  1. Uwe na umri kati ya miaka 18-45
  2. Uwe umehitumu katika vyuo vya ufundi stadi na kupatiwa cheti
  3. Uwe umehitimu katika mikopo ya PTF ya Pamoja Loan
  4. Uwe na shughuli za uzalishaji ama uwe tayari kuanzisha shughuli kulingana na masomo ya ufundi stadi uliyosomea
  5. Uwe na kitambulisho cha Taifa ama kadi ya mpiga kura
  6. Uwe na mahali maalumu pa kufanyia shughuli yako
  7. Uwe katika eneo la maradi wa PTF
  8. Uwe na historia nzuri ya ukopaji
Viwango vya Mkopo
  • Mkopo wa chini TZS 3,000,000
  • Mkopo wa juu TZS 10,000,000
  • Muda wa urejeshaji ni kati ya miezi 6-12

Mkopo wa Vifaa

Katika kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda. Mkopo huu unalenga kuwawezesha wanufaika wa Mfuko kuanzisha ama kuboresha miradi ya viwanda vidogo vidogo.

Vigezo vya Kupata Mkopo
  1. Uwe umehitumu katika vyuo vya ufundi stadi na kupatiwa cheti
  2. Uwe tayari kujiunga katika kikundi cha watu watano na kudhaminiana
  3. Uwe na shughuli za uzalishaji ama uwe tayari kuanzisha shughuli kulingana na masomo ya ufundi stadi uliyosomea
  4. Uwe na kitambulisho cha Taifa ama kadi ya mpiga kura
  5. Uwe na mahali maalumu pa kufanyia shughuli yako
  6. Uwe katika eneo la maradi wa PTF
  7. Uwe na historia nzuri ya ukopaji
Viwango vya Mkopo
  • Mkopo wa chini TZS 100,000
  • Mkopo wa juu TZS 5,000,000
  • Muda wa urejeshaji ni kati ya miezi 6-12

Mkopo wa Zabuni

Mkopo huu unalenga katika kuongeza tija katika miradi ya uzalishaji mali; kwa kuwawezesha wanufaika wa Mfuko kukidhi mahitaji ya haraka ya vifaa, pembejeo na kusambaza bidhaa kwa wanunuzi ndani ya muda wa mkataba wa huduma inayoitajika.

Vigezo vya Kupata Mkopo
  1. Uwe umehitumu katika vyuo vya ufundi stadi na kupatiwa cheti
  2. Uwe tayari kujiunga katika kikundi cha watu watano na kudhaminiana
  3. Uwe na shughuli za uzalishaji ama uwe tayari kuanzisha shughuli kulingana na masomo ya ufundi stadi uliyosomea
  4. Uwe na kitambulisho cha Taifa ama kadi ya mpiga kura
  5. Uwe na mahali maalumu pa kufanyia shughuli yako
  6. Uwe katika eneo la maradi wa PTF
  7. Uwe na historia nzuri ya ukopaji
Viwango vya Mkopo
  • Muda wa Mikopo: sio zaidi ya miezi 3
  • Kiwango cha chini cha mkopo kiasi cha 500,000 / =
  • Kiwango cha juu cha mkopo kiasi cha 5,000,000 / =
  • Muda wa urejeshaji ni kati ya miezi 3-6